GET /api/v0.1/hansard/entries/1270100/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1270100,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1270100/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, si vizuri kunyang’anywa mlinzi lakini ningependa kukumbusha Seneti hii kwamba kulikwa na maandamano Tarehe 7, Julai, 2023. Hakuna mtu aliye na macho ambaye hakuona vile Nairobi Expressway ilivyoharibiwa. Watu walipigana na wengine hata wakauawa kwa sababu hakukuwa na ulinzi wa kutosha. Baadaye, Azimio la Umoja ilitangaza siku tatu za maandamano. Naunga mkono kunyang’anywa kwao bunduki na walinzi kwa sababu ikiwa maandamano hicho kitu kingefanyika siku hiyo, basi hatungekuwa na nchi hii leo. Wale walionyang’aywa walinzi wangekuwa wamekaa katika mlima huu na wengine ule, Kenya ingechomeka. La pili ni kwamba, tulikuwa na Bi. Spika wa Muda Tarehe 6 Kikao cha jioni. Yale yaliofanyika katika Kikao hiki baina yake na Seneta wa Nairobi kingefanyika pale nje, basi watu wangeuana. Kwa hivyo, nauga mkono yale yaliyofanyika. Mwishowe, nawaona hapa leo kwa sababu hawana bunduki. Wangekuwa na bunduki, basi ungewaona hapo nje. Nakumbuka tulikuwa tunapitisha mambo mengi na haungewaona kwa sababu walikuwa na walinzi. Kwa hivyo, wangeenda hapo nje kurusha mawe, lakini wametulia hii leo. Hiyo ilikuwa ni funzo. Kwa hivyo, njooni tukae chini na tusemezane kidogo sisi kama Serikali ya Kenya Kwanza na Azimio la Umoja. Asante Bw. Spika."
}