GET /api/v0.1/hansard/entries/1270107/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1270107,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1270107/?format=api",
    "text_counter": 195,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii ili niweze kutoa kauli yangu. Kile ambacho nataka kusema ni kwamba, hao walinzi hawakuondolewa kwenu kinyume na sheria kwa sababu maandamano yalikuwa tayari yameharamishwa na taasisi husika la Taifa la Kenya. Hakuna Mkenya pahali popote ambaye hakupata ilani ya kuwa, maandamano yalikuwa yameharamishwa. Ni jukumu la Serikali kulinda wananchi pamaoja na mali ya raia wa Kenya. Ni jukumu la Inspector General (IG) wa Taifa la Kenya, kuhakikisha usalama. Hata ikiwa hao walinzi wenu wanawachunga nyinyi, wao pia wako na haki za Kikatiba ambazo zinastahili kulindwa. Mlinzi wao ndiye aliyewaambia wao wasije kuwalinda. Kwa hivyo, ningependa kusema kitu kimoja kama Mkenya. Tusiombe tupewe haki ambazo hatutaki kuchukulia majukumu. Our rights come with responsibilities ."
}