GET /api/v0.1/hansard/entries/1270817/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1270817,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1270817/?format=api",
"text_counter": 447,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Nami ninachukua fursa hii kumushukuru Mhe. Rahim kwa kuuleta Mswada huu Bungeni. Ninampongeza sana. Mhe. Spika wa Muda, katika Mombasa na Pwani, sisi tumekuwa watu ambao tunapitwa sana na mambo ya ajira. Watoto wetu wamesoma, wana stakabadhi zao na wamesoma mpaka masomo ya juu lakini wakati wa ajira ukifika, watoto wetu wanatengwa sana. Nimezunguka sana ndani ya Mombasa. Na hata wakati mwingine unaangalia hata kwenye magazeti, ajira imetangazwa, ambayo pengine ni ya pale ndani ya Pwani au Mombasa, ukienda unapata hata ilitangazwa, tayari walishachukua watu."
}