GET /api/v0.1/hansard/entries/1270818/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1270818,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1270818/?format=api",
"text_counter": 448,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Vijana wetu wameingia kwenye mambo ya pombe, mihadarati, na kwa mambo ya kukata watu vipanga na wachukue bibi na vitu vinginevyo kwa sababu wametengwa. Na ndiyo mimi ninataka nimpongeze Mhe. Rahim kwa kuuleta huu Mswada w a kuweza kuwawekea usawa Wakenya wote. Ikiwa mtoto wa Mombasa, magharibi mwa Kenya, au kutoka wapi, maadam anazo stakabadhi na uwezo wa kufanya kazi, apewe kazi. Kwa mfano, ndani ya Port ya Mombasa, watoto wetu wengi hawako pale. Unaona magari pengine yanafanya importation kwa sababu kuna mtu fulani ambaye anaongea lugha fulani na analeta watu wake tu. Anasahau kuwa uwiano ama Kenya tunaijenga kama moja bila kuangalia kabila au rangi."
}