GET /api/v0.1/hansard/entries/1270821/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1270821,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1270821/?format=api",
    "text_counter": 451,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Jambo hili limenipa jazba kubwa sana. Mheshimiwa mwenzangu pale amesema ajira ikitokea mahali popote pale, tusiangalie mtu ameletwa na nani. Tusiangalie huyu ni mtoto wa nani. Tuangalie ana uwezo wa kufanya kazi. Je, ana tajriba ya kufanya kazi? Je, anastahili kupata hii kazi? Kwa hivyo, ninaunga mkono kabisa mjadala huu haswa nikipigia upato watoto wetu wa kiume, wakike na wale ambao ni professionals katika kazi tofauti tofauti. Wakibisha mlango, itakuwa ni bora zaidi wale wanaohusika na ajira wafungulie kila mtoto mlango bila kuangalia kabila, umaskini ama utajiri. Waangalie karatasi zake na kama yuko sawa, basi apewe ajira."
}