GET /api/v0.1/hansard/entries/1270822/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1270822,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1270822/?format=api",
    "text_counter": 452,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Hili ni donda sugu katika taifa letu na ni Jumba hili tu linaweza kupigana na hali hii ngumu na kusawazisha mambo. Sheria inasema kuwa ikiwa ajira pengine ziko ndani ya Mombasa Port, 70 per cent inabaki kwa watu wa Mombasa, na 30 per cent yaweza kwenda ikatolewa kwa wale wengine. Lakini hii yote inabaki kuwa ndoto. Watoto bado wanakosa ajira. Mswada huu wa Mhe. Rahim umeletwa kusafisha mambo haya yote. Kama Mama Mombasa, leo ninaimani kwamba watoto wangu wakienda katika kaunti ya Mhe. Rahim wanaweza wakaandikwa kazi. Wakienda kule kwingine, madam wana stakabadhi zao, basi wanaweza wakaandikwa kazi. Ile hali ya kutengwa na mtoto anabaki kwao tu hajui kutoka nje kuunganishwa na Kenya nzima ndio imefanya hata sisi Wapwani tumeachwa pale pale tu."
}