GET /api/v0.1/hansard/entries/1270824/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1270824,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1270824/?format=api",
"text_counter": 454,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Ninazungumza nikiangalia Dongo Kundu inayokuja; hii imekondolewa macho na watu wengi sana. Lakini ni muhimu tujue kuwa kule Pwani kuna watoto ambao wamekaa miaka mingi na vibali vyao bila kazi. Ningeomba wale ambao watahusika katika Dongo Kundu wawangalie watoto hao katika sehemu hii. Ikiwa watataka plumber, electrician, mechanic, mpaka rangi, secretary au manager, basi waanze kuwatengea wale ambao wako kule katika ule mgao wao. Wawe na ile haki ya kuweza kutoa kazi kwa uhaki. Wawekee watoto wetu nafasi zao za kazi. Baadaye, wanaweza kugawanya zinazobaki kwa sababu tunataka kuaminiana vizuri kama taifa moja. Hayo yakifanyika, basi kama Wapwani tutashukuru."
}