GET /api/v0.1/hansard/entries/1270825/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1270825,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1270825/?format=api",
"text_counter": 455,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Jambo lingine ni kwamba, licha ya kuwa tunatafuta namna ya kuweka ajira sawa, ni jukumu la Serikali pia kuweza kuweka msukumo kuleta investors na kuongeza factories . Kule Pwani, tulikuwa na factory ya korosho lakini ilifungwa. Hizi ni sehemu ambazo zilikuwa zinatoa ajira kwa watoto wetu. Tulikuwa na factory ambayo ilikuwa inatengeneza pamba. Tulikuwa na pixa. Hizi zote zilifungwa. Kama Serikali inaweza kufungua hizi zote, basi nafasi za kazi pia zipatikane ili watoto wasiweze kung’ang’ania zaidi. Ninashukuru kwa mjadala huu na nampongeza sana ndugu yangu Mhe. Rahim kwa kuleta huu mjadala. Nina uhakika kuwa Mswada huu ukiweza kupita hapa, kila Mkenya anayetafuta ajira atapata haki yake kwa sababu sisi sote ni walipaushuru. Awe maskini, tajiri, Mluhya, Mswahili ama Mkauma, wote wanalipa ushuru na wanastahili kupata haki zao. Ninamalizia hapa nikishukuru sana na kusema kuwa ninaunga mkono Mjadala huu kwa nguvu zangu zote. Ninaomba Mwenyezi Mungu ili huu mjadala upitishwe katika Bunge hili ili tuweze kupata haki sawa za ajira kwa watoto wetu. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}