GET /api/v0.1/hansard/entries/1271421/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1271421,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271421/?format=api",
"text_counter": 573,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nichangia Hoja ya kuongezewa muda kwa Kamati ya Muda inayo chunguza mashaka kule Shakahola. Kwanza, nampongeza Mwenyekiti wa Kamati hii na wanachama wake wote nikiwa mmoja wao kwa kazi nzuri ambayo wamefanya mpaka sasa. Tumeweza kuzuru maeneo ya Shakahola mara mbili na tukaona hali ilivyokuwa kule. Tulipozuru sehemu za makaburi, tulipata mwili mmoja ambao ulikuwa umepatikana na ukawa unapelekwa katika hifadhi ya maiti kule Malindi. Kazi iliyofanyika ni kubwa, lakini kazi iliyobaki ni kubwa pia. Hii ni kwa sababu mpaka sasa, hatujaweza kujua kama makaburi ambayo bado yana watu yamekwisha au la kwa sababu, hadi wiki iliyoisha, bado miili ilikuwa inatolewa katika makaburi. Bw. Spika wa Muda, changamoto ni nyingi kwa hakika. Hii ni kwa sababu tukiangalia wale maafisa wa polisi waliyo wekwa kule kufanya kazi hizo na wale maafisa wa afya ni binadamu na wanafanya kazi ngumu. Watahitajika kupata ushauri kwa muda mrefu kwa sababu yale mambo wanayoyapitia kule sio mambo ya kawaida. Janga hili kwa hakika ni kubwa kwa sababu mpaka sasa nafikiri ni miili 450 imeweza kufukuliwa na mingi bado yako katika hifadhi ya maiti pale Malindi. Ni vigumu kuwatambua wale waliofariki kwa sababu miili mingine ilikuwa ishaharibika."
}