GET /api/v0.1/hansard/entries/1271423/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1271423,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271423/?format=api",
    "text_counter": 575,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Vile vile, kazi ya kutafuta Deoxyribonucleic Acid (DNA) pia ina changamoto kwa sababu hatuna vifaa vya kupima DNA hapa. Mpaka, ziwasilishwe Afrika Kusini ambako pia inachukuwa muda kuweza kuwatambua wale waliofariki na jamaa zao tofauti tofauti. Wengi ambao walienda kule Shakahola walibadili majina yao. Kama unaitwa Mohamed Faki, kule unajiita jina lingine ambalo hata kama umeweza kupatikana, jina lako na stakabadhi zako zinaonyesha majina tofauti na yale ambayo ulikuwa unajulikana nayo. Kwa hivyo, imekuwa ni vigumu kabisa kuweza kuwatambua watu wale na kuwaunganisha na familia zao ili waweze kuzikwa. Bw. Spika wa Muda, muda uliyokuwa umepeanwa ni miezi mitatu lakini kulingana na kazi ambayo ipo, muda huo hauwezi kutosha kwa sababu bado kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanywa. Tumeweza kufanya mkutano na Mkuu wa Sheria, Waziri wa Usalama wa Ndani, Mwandishi Mkuu wa Vyama yaani Registrar of Societies na wengi ambao wametoa habari nzuri ambazo zitasaidia kamati hii kuwa na mwongozo bora ambao utatumika kwa muda mrefu. Swala la kudhibiti makanisa ama taasisi za kidini ni swala ambalo limeibuka. Kama ilivyo kawaida, wakati watu wanaambiwa wadhibitiwe, inakuwa shida kwa sababu kila mtu anataka kupata uhuru wake. Lakini, kwa maswala ambayo yametokea Shakahola, hatuwezi kukaa tena kando tukiona kwamba jamii inateseka na inasambaratika tukitaka kulinda uhuru wa kuabudu. Uhuru wa kuabudu lazima tuuheshimu lakini lazima pia wale wanao tekeleza maswala haya waheshimu uhuru wa watu wengine. Tumetoa mfano wa Rwanda. Rwanda wameweza kudhibiti taasisi za kidini. Hii ni kwa sababu walikaa kidete wakasema kwamba hawawezi kuacha kila kitu kiholela. Wakakubali kwamba kuwe na sheria za kuweza kudhibiti mambo yale. Hapa kwetu lazima pia tuwe na sheria ya kudhibiti mambo haya. Hii ni kwa sababu tukiangalia mpaka leo, baadhi ya wale ambao waliokolewa kule Shakahola, wengine wamekataa kula chakula, wengine wanasema kwamba wanaendelea na kufunga. Inakuwa bado wanawatatiza maafisa wa usalama na wale ambao wanawaangalia ili wahakikishe kwamba wamerejea katika Jamii, ili waweze kuisaidia jamii na kuendesha maisha yao kama kawaida. Bw. Spika wa Muda, swala la haki za binadamu pia limeweza kuibuka mpaka sasa. Hii ni kwa sababu wale ambao walipatikana ni manusura. Bado walikuwa wamewekwa katika kambi ili waweze kupewa ushauri mwafaka, ili waweze kurejea kuishi kama kawaida na familia zao. Lakini hivi majuzi, nimeona maombi ambayo yalikuwa yameombwa mahakamani na Kiongozi wa Mashataka anayehudumia katika sehemu ya Pwani akisema kwamba, angependa watu wale wazuiliwe katika gereza la Shimo la Tewa. Sasa watoke Shakahola waende Shimo la Tewa ili waweze kudhibitiwa pale wasiweze kuonana na familia zao. Swala ambalo lilikuwa limeibuka ndio hata Kiongozi wa Mashtaka aweze kufanya maombi haya ni kwamba, kuna ujauzito wa kiholela unaweza kutokea kwa sababu wale watu walikuwa wanakutana kimwili. Kwa hivyo, inaweza kusababisha ujauzito ambao haukutegemewa. Lakini swala hilo sio swala rahisi kwa sababu, kumfungia mtu jela bila kufuata sheria ni makosa zaidi kuliko mwanamke kupata ujauzito ambao hakutarajia."
}