GET /api/v0.1/hansard/entries/1271425/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1271425,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271425/?format=api",
"text_counter": 577,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, ni swala ambalo linaibuka na pia ningependa Mwenyekiti, aliangalie swala hilo wakati tutakapo ongezewa muda kwa sababu ni tatizo ambalo litahujumu sheria zetu za kuhusu haki za kibinadamu. Nikimalizia, leo tukiwa katika chakula za mchana, tulikuwa na Seneta wa Kaunti ya Bungoma. Yeye pia alinieleza kwamba majuzi, kuna watu kama hao wamepatikana Nakuru. Walikuwa wanaelekea sehemu za Ethiopia kuenda kwa maswala kama haya ya Shakahola. Ni mambo ambayo bado yako, dini kama hizi bado ziko na fikra kama hizi bado ziko. Kwa hivyo, inafaa tuweze kumaliza swala hili na tuliangalie vizuri ili kuwe na msingi wa kuweza kutunga sheria za siku za usoni, kuhakikisha kwamba maswala kama haya hayarejelewi tena katika nchi yetu. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono kuongezewa muda kwa Kamati hii na tunaomba kwamba tukipewa muda huu, tuweze kuitumia vizuri zaidi kuhakikisha kwamba ripoti ambayo itatoka pale itakuwa ni ripoti ambayo itaweka msingi katika taifa letu kwa miaka mingi itakayo fuata. Asante Bw. Spika wa Muda, naunga mkono kwa kuongezwa kwa muda kwa kamati hii."
}