GET /api/v0.1/hansard/entries/1271534/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1271534,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271534/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Naunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Hamida, kuhusu kuzembea katika hospitali ya Kiambu. Hili jambo la madaktari pamoja na wauguzi wale wengine kuzembea katika kazi yao imekuwa donda sugu katika hospitali zetu. Kuna yule mtoto ambae Kamati yetu iliingilia na kuchunguza. Alikuwa amegongwa na jembe kwa kichwa, akazungushwa mahospitalini na mwishowe akaaga dunia. Wale madaktari walikua wakiangalia na hakuna jambo lolote walifanya. Bw. Spika, tumeripotiwa jambo lingine lililotendeka pale Kiambu. Kamati inayohusika inapaswa iangalie haya maswali kwa undani na waangalie ni jambo lipi linalosababisha mambo kama hayo. Je, ni ukosefu wa vifaa vya kutosha, uchache ama upungufu wa wauguzi ama ni ile watu kutojali wenzao? Bw. Spika, vile vile, nachangia Taarifa iliyoletwa kuhusu hospitali ya Mathare ambayo inashugulikia watu walio na shida za kiakili. Ukitembelea hospitali ile, utapata ni ndogo sana ili wagonjwa ni wengi sana."
}