GET /api/v0.1/hansard/entries/1271536/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1271536,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271536/?format=api",
    "text_counter": 67,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Maswali aliyouliza Seneta huyo ni mazuri sana. Ni madaktari wangapi wanaoshugulikia mambo ya akili wako pale. Wakati mmoja, ilipatikana kwamba hospitali yenyewe ilikuwa ni chafu, wagonjwa wamewachwa na uchafu umetapakaa kila mahali katika hosptali ile. Kwa hivyo, Kamati hii ya Afya ina jukumu muhimu ya kuzingatia ya kwamba hospitali zetu zinatekeleza mambo ambayo yanapaswa kutekelezwa kwa njia ambayo Wakenya watafurahia. Bw. Spika, sio hiyo pekee yake. Ukitembelea hospitali zingine kama ya Laikipia, utapata hospitali hazina dawa na watu wanaandikiwa dawa. Wagonjwa wanaambiwa hata ijapokua wana kadi za National Health Insurance Fund (NHIF), hospitali hazina dawa. Wagonjwa wanaohitaji kupiga picha, wanaelekezwa mahali fulani. Inakaa wale madaktari wanapata mlungula kwa sababu wanakuelekeza kwa duka fulani ya kununua dawa. Watu wanakisia ya kwamba hospitali zikipatiwa dawa na Serikali, dawa zinauzwa na kupelekwa pale nje kisha wananchi wanaambiwa waende kununua dawa hizo huko nje. Kwa hivyo, Kamati inayohusika iangalie haya mambo kwa undani na kuleta mapendekezo ya kudumu."
}