GET /api/v0.1/hansard/entries/1271538/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1271538,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271538/?format=api",
    "text_counter": 69,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Nampa kongole dadangu Sen. Kibwana kwa kauli aliyoleta Seneti. Tunaelewa ya kwamba, Wakenya wenzetu walio na akili punguani wanaenda hizo hospitali za akili punguani ili kupata matibabu. Lakini, tukiangalia zile sehemu zao za matibabu na vifaa vinayotumika kuwaweka katika yale maeneo, hali ya usafi na hali ya chakula, Serikali inafaa itafakari zaidi na kuhakikisha kuna madaktari wa kutosha ambao wana ile taaluma inayotumika kufanya hayo matibabu. Nilitembelea hospitali ya Port Reitz, eneo la Pwani. Matokeo tuliona kule yalikuwa hayafai hata kidogo. Hali ya usafi imepungua. Hali wanavyokaa wakati wanapokea matibabu, haiwezi changia watibiwe na kupona. Mtu, hata kama ana akili kidogo, akifika pale anazidi kuharibika. Bw. Spika, inatikikana tupate madaktari wenye taaluma ya kutosha, madaktari wa hali ya juu ili wakienda kukagua au kutibu wagonjwa wawe ni madaktari wanaweza kabisa kukabiliana na magonjwa kama haya ya akili punguani. Pili, ni upande wa malazi. Katika mahospitali haya yote tumeona, hata kule Mathare nimetembea na kushuhudia kwamba malazi yao yanakua mabaya sana. Hali ya afya na mazingira inakua ya kupungua kabisa. Saa zingine hata wakiitwa akili punguani, sijui kwa sababu gani, matibabu na hali yao ya kuweza kujikimu pale ndani inakua hali ya kusikitisha sana. Bw. Spika, naunga mkono kauli hii. Kauli iliyoletwa ni safi na inaweza pia kusaidia. La muhimu ni kwamba, majukumu kama haya au kuwa na hospitali za watu wenye akili punguani, inaweza pelekwa mahali kama Meru, kule kwa yule ndugu yangu, Naibu wa Spika. Huko kunahitaji pia. Mimi ninajua watu kama hao wenye akili punguani wako sehemu kama hizo."
}