GET /api/v0.1/hansard/entries/1271575/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1271575,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271575/?format=api",
"text_counter": 106,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13592,
"legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
"slug": "onyonka-richard-momoima"
},
"content": "Asante Bw. Spika. Ningependa kuchangia hili jambo ambalo Seneta kutoka kaunti ya Migori amechangia. Ninawasihi ndugu zangu wanaokaa kwenye Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili itakayoshughulikia hili jambo la mazingira ya Ziwa Victoria, --- Shida nyingi tulizo nazo sasa, zinahusu kuzingatia oboreshaji wa mazingira na kuhakikisha mito yetu ina maji. Tusipochunga Ziwa Victoria, huenda likaisha maji. Shida ni kwamba tumekua tukifanya haya makosa kwa miaka mingi. Kama sasa, Serikali imeamua kuwa jamaa wakate miti misituni. Wale tunaoishi karibu na hili Ziwa, tunajua kwamba miti ndiyo inaleta mvua. Hii miti ambayo imechungwa na serikali zote tangu nchi yetu ipate uongozi, ndio imekua ikileta maji kutoka upande wa juu. Katika Kaunti ya Kisii, tuko na maji siku 24 kwa siku 30 za mwezi, kwa sababu tuko upande wa juu wa Ziwa Victoria. Tumejaribu kuhakikisha miti inapandwa ndiposa mazingira ya Ziwa hili yasiharibike."
}