GET /api/v0.1/hansard/entries/1271587/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1271587,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271587/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "na maswala ya madhara ya mental hospital . Nikianzia hii ya pili ni kwamba ni ukweli matatizo ya afya ya akili imekuwa kidonda sugu. Utapata kwamba kama Maseneta waliotangulia walivyosema, vituo vya matibabu katika Kenya viko viwili pekee yake: Mathari na Port Reitz katika Kaunti ya Mombasa. Lakini hakujakuwa na uwekezaji wa kutosha katika taasisi hizi kiasi ambacho wengi wanaoenda pale wanateseka baadala ya kuangaliwa na madaktari ama wauguzi walio katika hospitali zile. Bw. Spika, tatizo kubwa pia ni kuwa kuna unyanyapaa katika familia za wale ambao wameathirika kwa sababu mtu wa akili pungwani mara nyingi huwa hausishwi kwa jambo lolote mpaka aanze kufanya fujo na kupigana ndiyo anapelekwa hospitali. Akifika hospitali, anawekwa huko na hapati matibabu ya kisawa sawa. Juzi nilibahatika kuenda katika hospitali ya Port Reitz. Cha kusikitisha ni kwamba mgonjwa wa akili akifika pale lazima kwanza alipe Kshs10,000 ndio aweze kupokelewa na ahudumiwe. Kwa hivyo, ningependa hii Kamati ya Afya pia izuru hospitali ya Port"
}