GET /api/v0.1/hansard/entries/1271617/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1271617,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271617/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante Bw. Spika. Kwa Hoja ya Nidhamu, ukiangalia tabia za wale Maseneta wengine walio hapa ni vizuri kutimiza zile Kanuni za Kudumu. Sen. Orwoba ametoka upande ule akafika hapa katikati na kupita badala ya kwenda kwa mlango na kuinama, ili aje upande huu mwingine kulingana na taratibu zetu. Jambo lingine vile vile, Sen. Miraj amefanya kitendo kama hicho hapa mbele yetu. Sijui kama wanafaa kuomba msamaha kwa vitendo walivyofanya ama wakirejelee ili walifanye sawa sawa."
}