GET /api/v0.1/hansard/entries/1271924/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1271924,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1271924/?format=api",
"text_counter": 49,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika na Asante Bi. Waziri kwa kujibu maswali vizuri. Sasa tunazungumzia mambo ya mito. Sijui kama katika mipangilio yako, unafikiria kuhusu mito ile mikubwa kama vile River Tana, ambayo ukifika sehemu za chini kama vile pwani, zinageuza mikondo. Sijui kama Wizara yako imepanga ama ina mipangilo ya kuhakikisha ya kwamba ile mito inaregelea mikondo yake ya kawaida. Ninasema hivi kwa sababu ukienda sehemu za Mathomba-bruk ukiwa unashuka Garsen, utakuta ya kwamba mto ni kama unaanza kugeuka tena na unataka budget ya kuhakikisha ya kwamba mto ule unaenda vizuri maanake kuna wananchi wengi sana ambao wanaishi pale and wanautegemea mto ule kwa chakula, maji na kuisi. Sijui kama kuna mipangilio maanake nimekusikia unaongea mambo ya mto wa Nairobi lakini kuna mito hii ambayo inasimamia maisha ya wananchi wengi sana. Tena ukiangalia uzunguni, ukienda kama River Thames kule London, utaona kuwa wamejengea ukuta huku na kule. Mto ule hauwezi kuanza kugeuza geuza mkondo. Lakini huku kwetu tunashangaa kwa sababu mito imekuwa vilevile ilivyokuwa miaka ya akina babu. Tumeziachilia na sasa kwa sababu ya ongezeko ya watu, inakuwa ni shida kufuata vile akina babu walivyokuwa wakifanya; kufuata mito. Sasa hivi, haiwezekani tena kwa sababu watu wamejenga nyumba zao ambazo wanaishi. Swali langu ni mipango gani ambayo uko nayo kuhakikisha ya kwamba ule mto unafuatizia vile ulivyo ili watu wasiteseke katika nyanda za chini. Na kama hauna mpangilio wakati huu, mimi ninakuomba kwa heshima, ututembelee, uje uone hali ilivyo katika Tana River na pengine katika budget yako, utafute namna ya kurejesha maji yale, haswa hiyo ya Mathomba-bruk. Waziri, tafadahali."
}