GET /api/v0.1/hansard/entries/1272174/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1272174,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1272174/?format=api",
    "text_counter": 299,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ningependa kuchukua nafasi hii, kwanza kumpa kongole Seneta wa Baringo, Sen. Cheptumo, ambaye alimaliza mwaka mmoja mbele yangu shuleni tukisomea sheria. Nampongeza kwa kuleta Hoja hii hapa kwenye Bunge la Seneti. Ukweli wa mambo ni kwamba, tangu Kenya ipate Uhuru tumekuwa na ukandamizaji wa kabila ndogo ndogo katika mfumo wa kisiasa na kiuchumi hapa nchini. Historia inatuonyesha kwamba mkoloni alipokuwa anatawala Kenya, Uganda na Tanzania, alichagua namna ya kuwatawala watu wengi kwa kuwapa nafasi za ofisi kubwa kubwa. Hawa walikuwa tu watu walioamua kufanya kazi na mkoloni. Kwa sababu ya hiyo, wakati mkoloni alipokuwa mamlakani, kuna Waafrika wengine wachache ambao walichaguliwa kuwa machifu wakubwa. Hapo ndipo walishirikiana na mkoloni kukandamiza Waafrika wenzao huku wao wakipata nafasi ya kujiendeleza kiuchimi na Serikalini. Bw. Spika wa Muda, Rais wa Kenya wa kwanza, Mzee Jomo Kenyatta, alipochukua mamlaka, hakubadilisha mwelekeo huo. Hii ndio maana wengine walisema mzungu mweupe aliondoka lakini mzungu mweusi akaja. Ni kwa sababu mambo mengi hayakubadilishwa. Kabila ndogo ndogo ziliendelea kukandamizwa. Ndio maana ni muhimu leo tuizungumze Hoja hii. Sisi ambao tunatoka katika kabila ndogo ndogo, lazima tuyaseme haya ili tuelewane ya kwamba Kenya hii tuko na tunaishi. Tuko hapa na hatuondoki. Hawakugeuza haya bali waliendelea vivyo hivyo. Ukandamizaji huu ulielekezwa kwamba nafasi za kiserikali kwa watu wa Tana River miaka ya Mzee Jomo Kenyatta ilikuwa chache. Sehemu zile za watu wengi ndio walipata nafasi. Vile mkoloni alivyokuwa anafanya, ndivyo Rais wa kwanza alifanya. Bw. Spika wa Muda, ukiangalia upande wa masomo na watu waliosoma hadi chuo kikuu, Rais wa pili pia alifuata nyayo za hayati Jomo Kenyatta. Yeye mwenyewe alisema: “Mimi nitafuata nyayo za Rais Mzee Jomo Kenyatta” na kweli alifuata nyayo. Alichukua uongozi ule ule na kufanya vile vile. Makabila madogo yalishushwa na kuendelea kukandamizwa. Ukiangalia majedwali na hata utafiti ambao umefanywa kwa vyuo vikuu, utaona ya kwamba makatibu wa kudumu, wakubwa wa mashirika ya kiserikali na wafanyikazi wa kiserikali, utakuta nafasi za wale kutoka makabila madogo"
}