GET /api/v0.1/hansard/entries/1272176/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1272176,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1272176/?format=api",
"text_counter": 301,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "zilikuwa chache sana. Ilifika wakati ambapo katika kitengo kizima cha Serikali ama shirika la Serikali, watu wanaongea lugha ya kinyumbani. Hoja hii ni muhimu sana. Ili watu waanze kuelewana, tujaribu kugeuza mambo ambayo yamekuwa donda sugu katika hali ya uchumi na kisiasa hapa Kenya. Rais wa tatu ambaye tunamsifu sana, alijaribu lakini mambo yale yale yaliendelea. Rais wa nne, vivyo hivyo. Tulipopata hii Katiba mpya na vile vipengele vyote ambavyo Sen. Cheptumo amevitaja, Katiba hii mpya inasema tujaribu kuleta mabadiliko katika hali ya usimamizi, uchumi, nafasi za kiserikali na hali ya usimamizi katika mashirika ya kiserikali. Ilikuwa kwamba makabila madogo yahusishwe katika Serikali. Tunajua mabadiliko yanaendelea na tunajaribu kuyazungumza haya ili yawe katika akili za wale watu ambao wako na nafasi Serikalini kwa wakati huu. Tunachukua nafasi hii kupitia Hoja hii, kusema wazi wazi ya kwamba mawaziri ambao wamechaguliwa katika ofisi zao waanze kuzitatua shida hizi. Leo, Seneti inasema waanze kuzitatua namna hii; waziri akiwa na nafasi ya kuchagua watu moja kwa moja, yani watu ambao anachagua kwa mkono wake, usichague watu wa kabila lako pekee. Tuwaomba wajaribu kubadlisha hali ya mambo kwa kuweka hali ambayo inafaa katika wizara zao kwa sababu wakianza kushuka, makatibu, directors na watu wa ngazi za chini watafuata. Tunataka Mawaziri wakiwa Serikalini waangalie wale ambao wanachukua nafasi katika organizations za serikali kwa kuwahusisha watu kutoka makabila madogo. Saa hizi ukiangalia, Tana River, hakuna hata managing director mmoja katika"
}