GET /api/v0.1/hansard/entries/1272178/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1272178,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1272178/?format=api",
"text_counter": 303,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "yoyote ya Kenya tunavyoongea. Tana River saa hii, tunaangalia na watu wanaangalia na wanaona machungu yako na haya mazungumzo lazima tuyasema iliwanaosikia wajaribu kubadilisha mambo haya. Tunangojea kuona iwapo pengine wale ambao wameshika nafasiza kazi--- Tangu uhuru, hatujapata waziri kamili. Mimi mwenyewe nimetumikia kama waziri msaidizi lakini waziri kamili hatujapata kutoka Kaunti ya Tana River. Ninajua kaunti zingine pia hawajapata lakini tunasema mabadiliko yafanyike. Tunawaomba wale walio mamlakani wabadilishe mambo haya ili sisi sote tujisikie tu Wakenya. Lakini hata baada ya kupitishwa kwa Katiba hii ambayo ilileta gatuzi 47, tumepata shida hata sehemu za magavana. Shida ambayo imepatikana ni kwamba, magavana waligeuza maneno sasa na wakataka kuwa kama marais na kujiita HisExecellency . Mwanzoni ilikuwa shida lakini mwishowe, ikawa tumekubali sisi sote Kenya tunawaita His Excellency kama Rais. Hata hivyo, wao pia wakaanza kuiga mifano ya marais wa zamani kwamba watachukua kabila zao na kuziweka katika serikali. Kwa kufanya hivyo, watu kutoka makabila madogo yametengwa kutoka kwa serikali za kaunti. Katika Gatuzi la Tana River, Gavana alishtakiwa kwa sababu mwananchi alisema kuwa kuna sheria ambayo imevunjwa. County Government Act, inasema kabisa, lazima zile nafasi zigawanywe lakini magavana hawafuati sheria hiyo. Haya maneno lazima tuyazungumze. Leo ukiwa Nairobi, pengine kabila hilo ni kubwa lakini ukifika kwa"
}