GET /api/v0.1/hansard/entries/1272180/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1272180,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1272180/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "gatuzi ya Tana River, utakuta kabila hilo ni ndogo. Lakini hao ni Wakenya kama Wakenya wa huku. Tunataka tuwe na moyo wa kubadilisha hali ilivyo sasa. Hoja hii ambayo iko mbele yetu, tunataka kuzungumzia jambo hili. Nyumba ambayo mambo yanajadiliwa na kupangwa kama wazee, ni hapa. Tunatuma ujumbe kwa magavana wote ya kwamba waiangalie Kenya kama nchi yao. Usitambue watu wale ambao walikupigia kura au kabila lako pekee. Unapotengeneza serikali yako na kujaza nafasi za Mawaziri na Makatibu wa Kudumu, tafadhali, angalia ujue ya kwamba kuna Wakenya wengine haswa makabila madogo madogo. Ukiangalia leo Kaunti ya Tana River, utaona makabila madogo madogo. Makabila yetu makubwa ni Wapokomo, Waoromo na Wardei. Hata hivyo, kuna makabila kama Wata, Wagiriama, Wakikuyu, Walwana na Wanyoyaya ambao ni wachache pale. Katika serikali ambayo inaundwa na County Public Service Board (CPSB), ni nafasi chache sana ambazo zinaenda kwa yale makabila madogo. Wakati mwingine, yale makabila makubwa yanaegemea upande mmoja. Yakifanya hivyo, yanaegemea zaidi kwa"
}