GET /api/v0.1/hansard/entries/1272182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1272182,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1272182/?format=api",
    "text_counter": 307,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "fulani ya kabila hilo. Ni lazima tabia hizi mbaya za kisiasa zikome. Ni lazima tusimame kwa umoja hapa Seneti na tuseme kwamba mambo ya kuwatenga watu wetu kutoka Serikali ya kitaifa na serikali za ugatuzi yaondolewe. Tuzungumze mambo ya umoja nchini Kenya na katika magatuzi yetu. Isiwe kwamba mtu akitoka kaunti hii hawezi kuenda kuishi katika kaunti nyingine kwa sababu hakuna nafasi kule. Mtu asiamue kwenda kuishi Uingereza kwa sababu hawezi kupata nafasi kubwa hii Kenya hata awe na talanta ya aina gani. Hivyo tunavyosema kuhusu Serikali ya kitaifa ndivyo tunavyotaka katika magatuzi zetu, kuwe na haki na usawa. Hii ndiyo Hoja ambayo iko hapa mbele yetu. Ninamshukuru Sen. Cheptumo kwa kuwasilisha Hoja hii hapa kwa sababu ni lazima tuyazungumzie. Kidonda kikiwepo, kama hakiwekwi dawa, basi hakiwezi kupona. Wakati mwingine ukiweka dawa kwenye kidonda, unasikia uchungu. Miaka zile tulipokuwa wadogo tulikuwa tukipakwa dawa ya samawati inayoitwa ‘ Jivi’ . Ukipakwa dawa hiyo unawashwa kabisa lakini hivyo ndivyo kidonda hupona. Ni lazima tuambiane ukweli. Kujenga Kenya hii iwe na sauti moja, basi ni lazima tuwe na usawa katika kabila zote ambazo ziko katika magatuzi zetu na Serikali ya kitaifa. Hivyo ndivyo wananchi wanavyotarajia. Si kwa makabila pekee lakini pia kwa nafasi za Serikali za kuwekeza na kujenga uchumi. Tuwe na umoja wa ukweli katika magatuzi zetu na Serikali kuu na sio umoja wa mdomo. Bw. Spika wa Muda, ningeomba Maseneta wote ambao watachangia Hoja hii ya Sen. Cheptumo waongee ukweli. Tuunge mkono maombi ambayo yako kwenye Hoja hii ili Wizara na sehemu za Serikali ambazo zinahusika zilete mabadiliko ya kisheria na miungomisingi ambayo itasaidia Kenya iwe na umoja."
}