GET /api/v0.1/hansard/entries/1272724/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1272724,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1272724/?format=api",
"text_counter": 179,
"type": "speech",
"speaker_name": "Juja, UDA",
"speaker_title": "Hon. George Koimburi",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipea nafasi hii ili nichangie jambo la ugonjwa wa cancer ambao umeleta shida katika taifa letu la Kenya. Ninaomba Waheshimiwa wenzangu tujaribu kuliangalia kwa undani zaidi kwa sababu mwenye ameleta Hoja hii aliongea juu ya Hazina inayoweza kutumika katika matibabu ya ugonjwa wa cancer. Hili jambo ni la muhimu na lizungumziwe katika Jamhuri yetu ya Kenya kwa sababu watu wengi wameumia na kufilisika. Familia nyingi zimezorota. Watu wameuza mashamba, nyumba, na raslimali ambazo zingefaidi jamii zao. Kwa hivyo, ninaomba tuliangalie jambo hili tukiangazia sana pahali pesa hizi huwa zinaenda na tuhakikishe zinarudishwa kwa raia na zisaidie watu haswa kujenga hospitali na kupeana madawa ambayo yatasaidia kutibu ugonjwa wa cancer. Asante sana Mhe. Spika wa muda."
}