GET /api/v0.1/hansard/entries/1272743/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1272743,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1272743/?format=api",
"text_counter": 198,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": "Jibu la tiba ya saratani liko kwa Waafrika. Jamii ya Magharibi ni nzuri sana kwa kubuni matatizo, lakini sio kutoa suluhisho. Lakini jamii ya Afrika ina suluhisho. Tunaweza kulizuia na kulimudu suala hili la saratani. Ningependa kumshukuru ndugu Timothy kwa kuleta Hoja hii ya kuweza kubuni hazina maalum ambayo itashugulikia suala hili la saratani. Kwanza, Hazina hii itatusaidia kufanya utafiti. Vilevile, itasaidia wale ambao hawawezi kugharamia matibabu haya ya saratani. Saratani ni ugonjwa ambao unaweza kudhibitiwa kwa wakati unaofaa."
}