GET /api/v0.1/hansard/entries/1272752/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1272752,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1272752/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Nilikuwa ninaelezea shida ambayo inatukumba. Kwanza, sio wahusika wengi hujitokeza kufanyiwa uchunguzi. Hii ni kwa ajili ya hofu ambayo imewekwa pale. Ukweli ni kwamba tunaweza kuzuia na kumudu ugonjwa huu wa saratani. Bunge hili limebahatika kwa sababu tuna mahali pa mazoezi. Kuna sehemu ya reflexology . Ni sehemu muhimu ambayo hata kama ugonjwa utakuandama siku chache zijazo, kwa njia ya reflexology, unaweza ukajulikana unaenda kuandamwa na ugonjwa upi. Saratani ya aina yeyote pia inaweza kugunduliwa hata kama inaanza saa hii kwa kutumia ile njia ya reflexology . Hivyo basi, ikiwezekana, katika mafunzo ya udaktari, reflexology iweze kujumuishwa kwa sababu ni kitengo muhimu ambacho kinasaidia kujua magonjwa ya aina mbalimbali. Reflexology inafanya kazi sawa na ile mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI). Hivyo basi, ningehimiza wizara husika ihakikishe kwamba somo hili linafundishwa katika vyuo vyetu vya udaktari. Tukifanya hivyo tutaweza kusaidia jamii yetu kwa kukinga na pia kudhibiti ugonjwa huu wa saratani. Kuna pia shirika la ubora wa bidhaa ambalo kwa sasa linatubwaga. Tunavyozungumza, asilimia sitini ya madawa yanayouzwa na kutumika hayafai kabisa. Ni asilimia arubaini tu ndiyo madawa ambayo yanaweza kutufaa kwa matumizi. Sitini hayafai na bado yanapatikana kwenye maduka ya kuuza madawa. Shirika hilo linafaa lipigwe msasa."
}