GET /api/v0.1/hansard/entries/1272773/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1272773,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1272773/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Kwa sababu ya wakati, nitazungumza kwa haraka. Jambo la kwanza, ni kumshukuru ndugu yangu, Mhe. Timothy Toroitich kwa sababu hili swala la saratani, ni jambo ambalo linagusa kila Mkenya kwa njia moja au nyingine. Na ninapozungumza, ni jambo ambalo liko karibu sana na moyo wangu. Ningependa kuunga mkono hii Hoja. Kwa kweli, tunafaa kuweka kitita cha hazina, ili sisi kama Wakenya, tuweze kujikinga na kudhibiti ugonjwa wa Saratani maana, ni jambo ambalo litaweza kutusaidia mahali pakubwa sana."
}