GET /api/v0.1/hansard/entries/1273593/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1273593,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1273593/?format=api",
    "text_counter": 41,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa nafasi hii kutoa mawazo yangu kuhusu Petition hii amabayo iko mbele yako. Swala la ardhi sehemu ya Pwani limekua donda sugu kwa wakaazi wa Pwani. Kati ya ahadi ambazo Serikali hii ya Rais Ruto ilitoa ni kwamba, watalimaliza hili swala na kupunguza shida za wananchi sehemu ya Pwani. Ukweli usemwe kwamba katika safari za Rais na Mawaziri wake, tumeona dalili ya swala hili kutatuliwa. Ni jambo la kusikitisha sana kusikia kwamba sehemu ya Mghange, Kaunti ya Taita-Taveta, wananchi wengi wanakosa ardhi kwa sababu kuna shamba kubwa ambazo zimeshikiliwa na mabwenyenye. Bw. Spika, tunashangaa sana kusikia kwamba kanisa na wananchi wanakosana kuhusu ardhi yao ya tangu jadi. Kwa hivyo, tunataka Kamati ya Ardhi kupitia mwenyekiti wao, walichukulie swala hili kwa uzito. Sehemu ya Pwani ina rekodi mbaya kuhusu watu kunyang’anya watu wengine mashamba. Watu ambao ni wachochole na ambao hawana nguvu, wananyang’anywa mashamba yao ama kukoseshwa haki zao za kiardhi. Kwa hivyo, nasimama kuunga hii Ardhilhali. Naomba Kamati husika itatue swala hili kwa haraka sana. Ningependa pia wakati Kamati hiyo inaangalia hili swala, nawaomba sana watembelee sehemu hiyo. Hii ni kwa sababu Mghange ni sehemu ya milima. Ukisikia mtu amechukua ekari 1,000 katika sehemu hizo za milima, basi wale Wananchi wamebaki na mahali pachache sana. Kwa hivyo, tunaomba Kamati husika wafanye hii kazi na watembelee sehemu za Mghange. Wasifanye kazi Nairobi tu bali waende wajione wenyewe hali ya maisha ya wale Wataitata ambao wanaishi huko juu."
}