GET /api/v0.1/hansard/entries/1274044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1274044,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1274044/?format=api",
    "text_counter": 492,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, kwa mujibu wa Kanuni 105 ya Kanuni za Kudumu za Seneti, lazima Seneta awajibike kwa matamshi yake. Sisi kama Maseneta na viongozi wa Kenya Kwanza tulikula kiapo kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba na kuhakikisha ugatuzi unafanya kazi. Sen. Osostsi hawezi kujilimbikizia heko kwamba kama siyo wao, kaunti zetu hazingepata pesa. Hiki ni kinaya kwa sababu sisi kama Walio wengi katika Serikali tuna vikao vya mara kwa mara na Mhe. Rais. Haya ndio masuala sisi hujadili kwa minajili ya kusukuma ajenda ya maendeleo za gatuzi zetu. Naomba asiwe wa kujipiga upato kwa sababu hata hapa Seneti wengi wa Walio wachache hawapo. Sisi tunavumilia kuwasikiza na kuwafanyia mema Wakenya waliotupigia kura. Naomba Sen. Osotsi atoe thibitisho kwamba walifanya mikutano mpaka asubuhi ili Wakenya wapate pesa. Jambo la mwisho, ni lazima Sen. Osotsi afurahi kwamba sisi ni wachapa kazi ambao tunawapenda Wakenya wote. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}