GET /api/v0.1/hansard/entries/1274068/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1274068,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1274068/?format=api",
"text_counter": 516,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, naunga mkono jambo hili linalohusika na bajeti. Pia naunga mkono Serikali ya Kenya Kwanza kwa kazi inayofanya. Kwa miaka mingi kumekuwa na shida na bajeti ya Kenya. Hii ndiyo bajeti ya kwanza ya Serikali ya Kenya Kwanza. Pia naunga mkono Wizara ya Fedha kwa kazi ambayo imefanya katika mwezi huu wa saba. Kwa mfano, ninaona Embu kwa mwaka moja tumepewa pesa billioni 5.34. Mwezi wa saba tumepata millioni 454. Tumetaabika kwa miaka mingi. Naunga mkono kwa sababu sasa hakutakuwa na deni. Kila mwezi mipango ya kaunti itakuwa inaendelea vizuri. Mnajua ya kwamba kaunti zetu ziko na shida ya mambo ya elimu, ukulima, mijengo na maji ya kilimo. Nashangaa sana kusikia watu wengine wakisema tulipitisha pesa kidogo ilhali wakati tulipokuwa tukijadili mambo haya yote, hawakuwa katika kikao hiki. Mlikuwa mmeenda kutupa mawe. Kwa hivyo, nataka niwaambie sio wakati wa kuleta vita. Ni wakati wa kuenda kuangalia kaunti zetu na magavana wetu wanavyofanya kazi. Kwa mfano, kama nina agano nawe kuwa nitakupa shilingi milioni kumi alafu nije nikuambie nina shida nipe milioni moja, hautaona makosa ya kunipa pesa hizo kwa sababu unajua nitarudisha. Kilicho muhimu ni kuwa usinipe pesa zote. Ninaunga mkono mambo haya. Pia naunga Serikali ya Kenya Kwanza mkono. Inaonekana ina mpango mzuri. Tutakuwa tunapokea fedha hizi kila mwezi. Hivyo basi, hakutakuwa na madeni. Asante Bw. Spika wa Muda."
}