GET /api/v0.1/hansard/entries/1274542/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1274542,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1274542/?format=api",
"text_counter": 356,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": "Ningependa kukurudisha nyuma kidogo. Kama utakumbuka, kuna wakati kulikuwa na hali kama hii kule Turkana na Pokot. Tulisafiri, kama Wabunge, na kushiriki katika michezo pamoja na jamii hizo mbili. Kama utakumbuka, siku hiyo wale waliokuwa wameiba mifugo ya wengine, walirejesha mifugo hao. Hatimaye, baada ya hapo, hatukusikia tena visa kama hivyo. Lakini miaka michache iliyopita, visa hivyo vilikithiri sana. Mhe. Spika wa Muda, ukiwa mmoja wa wanamichezo, naona kuna haja ya kurudi tena Turkana, Pokot na kule Kapenguria ili kujaribu kusawazisha na kuwaonyesha kwamba Kenya ni moja, na hatustahili kupigana wenyewe kwa wenyewe."
}