GET /api/v0.1/hansard/entries/1274543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1274543,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1274543/?format=api",
    "text_counter": 357,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": "Zaidi ya yote, usalama wa nchi uko na wananchi wenyewe. Usalama wa mtu uko na mtu mwenyewe. Jamii hizi mbili zinazozozana sana sana, usalama uko mikononi mwao. Iwapo watajitokeza kukaa na kuzungumza kwa amani, hakika amani itakuwa juu yao. Lakini, kama hali vile ilivyo, Hoja kama hii ikiletwa, wengi wao, hasa wale wanaohusika, huwa wanapotea. Hawakai kusikiza yale machungu ambayo wenzao wakonayo. Laiti wengine wangekuwa humu ndani wakaona yule Mheshimiwa akilia, hata wao pia pengine wangeingiwa na huzuni na kubadili nia zao."
}