GET /api/v0.1/hansard/entries/1274634/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1274634,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1274634/?format=api",
"text_counter": 78,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kathuri",
"speaker_title": "The Deputy Speaker",
"speaker": {
"id": 13590,
"legal_name": "Murungi Kathuri",
"slug": "murungi-kathuri"
},
"content": " Naomba Sen. Faki asikizwe bila hitilafu yoyote. Utalii ni kati ya sekta za uchumi ambazo zinachangia pakubwa pesa za kigeni kuingia nchini. Jambo la kusikitisha ni kwamba utalii umewachwa nyuma katika sekta zile ambazo zitachangia kufufua uchumi wa Kenya. Wengi wa wageni wanaoingia nchini, wanakuja kupitia Jomo Kenyatta International Airport, Nairobi . Tulileta Kauli kuhusiana na kufunguliwa kwa anga huru. Ni jambo kubwa kwa sababu, watalii wengi wanaenda Zanzibar ambayo inapakana na Kenya. Kuna ndege karibu 17 zinazotua kule kila siku. Ndege hizi zinapeleka biashara na watalii. Tukiweza kufungua anga huru kwa kaunti ya Mombasa, Kaunti ya Kilifi tufunguliwe Malindi International Airport, Kaunti ya Kisumu tufungue KisumuInternational Airport ; Kaunti ya Kwale tuinue uwanja wa Ndege wa Ukunda; Kaunti ya Uasin Gishu turuhusu ndege mpya za abiria katika uwanja wa Eldoret, uchumi wetu na utalii pia utainuka pakubwa. Uchumi wa Zanzibar hutegemea ufuo wa bahari. Hapa"
}