GET /api/v0.1/hansard/entries/1274636/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1274636,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1274636/?format=api",
    "text_counter": 80,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kathuri",
    "speaker_title": "The Deputy Speaker",
    "speaker": {
        "id": 13590,
        "legal_name": "Murungi Kathuri",
        "slug": "murungi-kathuri"
    },
    "content": "nchini tuna fuo za Bahari. Wanyama pori, hutoka Mombasa mpaka Taita Taveta kwa ndugu yangu Sen. Mwaruma. Ni safari ya saa moja pekee yake. Tukienda Kwale kwa Sen. Boy na Sen. Chimera, kuna fuo nzuri za bahari na wanyama pori katika Mbuga za Mwaluganje na kwingineko. Wale ambao wana shida za kushika nyumba kama Sen. Cherarkey watapata pweza na ngisi katika eneo la Kwale ili kuamsha mishipa ili aweze kujipa dawa vizuri. Swala la utalii ni muhimu sana kwenye Kaunti zetu. Hii ndiyo njia kubwa ya kuweza kuinua uchumi wa Mombasa na pwani nzima. Kutoka Lamu mpaka Shimoni kuna fuo za bahari. Kuna wale waliosema kuna simba wanaogelea kwenye sehemu ya Lamu. Tunajaribu kujenga uchumi wetu na tuweze kuinua utalii katika eneo letu la pwani. Asante kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ambayo imeletwa na dada yetu Sen. Okenyuri."
}