GET /api/v0.1/hansard/entries/1274665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1274665,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1274665/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii nichangie Kauli iliyosomwa na dada yangu, Sen. Okenyuri. Tarehe 24.4.2023, niliitisha Kauli isemayo: Kwanini anga ya Moi International Airport hairuhusu ndege za kimataifa kutua moja kwa moja? Ninashukuru kwa sababu juma lililokwisha, Rais William Ruto pamoja na Waziri wake wa Miundo Misingi, Mhe. Murkomen, walizuru Pwani. Baada ya ziara hiyo, walitangaza ya kwamba wamefungua anga ya Mombasa ili utalii ushamiri katika majimbo yote ya Pwani. Dada yangu Sen. Okenyuri, Mwenyezi Mungu akubariki. Sisi Wapwani tunategemea sana utalii. Utalii ndio uti wa mgongo wa uchumi wa majimbo ya Pwani. Ndiposa nimeona tunapofika hapa, sisi sio waakilishi tu wa yale maeneo tuliyotoka, bali waakilishi wa Taifa la Kenya. Kuona kwamba Mjumbe kutoka Kisii anajali wananchi na raia wenzangu wa kule ufuo wa Pwani, inanifariji roho. Hilo linaonyesha ya kwamba sisi kama taifa, tunapendana licha ya upungufu wetu na mikwaruzano ya kisiasa. Ningependa tena kumpongeza Rais wangu kwa kuifungua anga kupitia kauli yangu. Hiyo ni kumaanisha ya kwamba sisi kama Bunge, hatuko tu hapa kuuliza kauli. Ni wazi kwamba hizo kauli zinafanyiwa kazi na Executive. Mwenyezi Mungu akubariki dada yangu Sen. Okenyuri. Asante."
}