GET /api/v0.1/hansard/entries/1274678/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1274678,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1274678/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Naibu Spika. Wakati mwingine ni vigumu sisi sote kuelewa Kiswahili. Hata mimi pia bado ninajifunza Kiswahili. Sikusema “azilimia” bali nilisema “asilimia.” Kwa hivyo, nadhani amenielewa. Kitu ambacho nilikuwa nataka kusema ni kwamba, vijana walikuwa wakipata ajira hapo zamani. Lakini hivi sasa, ukiangalia hali ya uchumi na utalii katika nchii hii, haswa tukizingatia sehemu zote za pwani, utapata kwamba hoteli zimefungwa na vijana wamerudi nyumbani. Kile ambacho nasema ni kwamba, inatakikana kuwe na mikakati bora, kulingana na Taarifa iliyoletwa na Sen. Okenyuri, ili utalii uweze kurudi. Katika Kenya, tulikuwa na Utalii College na colleges zingine ndogo ambazo zimekuwa zikizingatia mambo ya utalii. Kulikuwepo pia na Ronald Ngala Tourism University ambayo ilikuwa pale Vipingo. Serikali ilianzisha huo mradi na ulikuwa mradi mzuri sana. Lakini, imepita miaka 18, kufikia hivi sasa, na hicho chuo kikuu bado hakijamalizwa. Serikali hii iliyoko kwenye mamlaka sasa inafaa ifanye juhudi zote ili chuo kikuu cha Ronald Ngala kimalizwe kujengwa kwa sababu kitasaidia watoto wetu kutoka kila sehemu ya Kenya ambao wanataka kujifunza taaluma ya utalii. Mwisho, tumekuwa tukisema hapa kila siku ya kwamba ni lazima tupanue airport zetu, ili ziwe kubwa na za kisasa. Tunafaa tuwe na viwanja vya ndege ambavyo ndege zinaweza kutoka nchi kama Italy na kutua kule Nandi ikiwa kutakuwa na airport kule Nandi. Vile vile, Malindi International Airport, mpaka hivi sasa, iko vile ilivyokuwa miaka kumi iliyopita. Ikiwa itaweza kupanuliwa, basi tutapata watalii kutoka Italy hadi Malindi. Ni lazima tuwe na mikakati ya kuongeza mambo ya utalii hususan tufikirie mambo ya Malindi International Airport. Bw. Naibu Spika, tumekuwa tukizungumzia mambo ya Lamu kila siku. Lamu iko nchini mwetu. Lamu ni mji wa utalii. Sehemu hiyo inawakilishwa na Sen. Githuku. Anasema---"
}