GET /api/v0.1/hansard/entries/1274770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1274770,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1274770/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Naibu Spika. Kwanza, ninaipa kongole Kamati yetu ambayo inajihusisha katika mambo ya mkasa wa bomu wa mwaka 1998 katika Ubalozi wa Amerika. Wakenya wengi waliathirika na majeraha na wengine kufa. Juzi nikitizama runinga, niliona mtu ambaye wakati huo alikuwa miezi saba tu tumboni mwa mama yake. Mama yake aliathirika katika huo mkasa wa bomu. Watu wengi walipata majeraha. Lakini wafanyakazi wa lile jumba la Amerika, kwa sababu ya sheria zao na mienendo yao ya kibinadamu, ilibainika wazi ya kwamba wale walioathirika na wale waliopata majeraha makubwa, walilifidiwa. Walifaidika ijapokuwa walipoteza watu wao na wengine kupata majeraha. Ile bomu haikulenga Mkenya yeyote bali Ubalozi. Hata hivyo, Wakenya waliokuwa wanafanya kazi zao waliathirika na hii bomu. Ingekuwa vyema ikiwa roho ya imani itawaingia Waamerika na walipe watu wetu ambao walijeruhiwa na wengine kupoteza wapendwa wao."
}