GET /api/v0.1/hansard/entries/1275164/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1275164,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1275164/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu wa Spika, ninamshukuru Waziri wa Elimu kwa ile kazi ambayo anaendelea kufanya katika kaunti zetu 47. Tunamuunga mkono. Swali langu linahusu walimu ambao hawajiwezi na wanaojiweza. Wanapofika miaka 60 na kustaafu, kunakuwa na shida za malipo. Kampuni nyingi zinalipa pesa za uzeeni baada ya miezi tatu. Lakini, upande wa elimu, wanakaa mwaka mmoja au miwili bila kulipwa pesa zao baada ya kustaafu. Tunaomba Waziri wa Elimu, aungane na Wizara ya Fedha ili tuweze kuinua uchumi wa Kenya na kuwasaidia walimu walipwe bila shida. Wanakaa muda mrefu mpaka wanabadilika, wanakaa kama vilema na wengine wanakufa. Ni kwa sababu mtu alikuwa anapata pesa na sasa ana shida. Atatoa suluhisho gani wakati huu kwa sababu Serikali ya Kenya Kwanza inafanya kazi nzuri?"
}