GET /api/v0.1/hansard/entries/1275541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1275541,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1275541/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu 53(1) za Seneti kuomba taarifa kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Barabara, Uchukuzi na Makao, kuhusu barabara zinazomilikiwa na mamlaka ya Kenya UrbanRoads Authority (KURA) katika Kaunti ya Mombasa. Katika taarifa hiyo, Kamati iangazie yafuatayo- (1) Iarifu Seneti ni barabara ngapi shirika la KURA limeweza kurekebisha kutoka mwaka wa 2018 hadi 2023 katika Kaunti ya Mombasa, ikiorodhesha majina ya barabara hizo kikamilifu; (2) Ichunguze matumizi ya fedha zilizotengwa kwa urekebishaji wa barabara hizo, ikizingatiwa kwamba baadhi ya barabara zilizo chini ya mamlaka ya KURA hazija rekebishwa kikamilifu; na, (3) Ieleze sababu zinazopelekea KURA kutumia wanakandarasi kutoka Kaunti ya Nairobi kukarabati barabara za Mombasa, ilhali wapo wanakandarasi wenye ujuzi na tajriba ya kutosha katika Kaunti ya Mombasa ambao wanaweza kufanya kazi hizo. Asante, mhe. Spika."
}