GET /api/v0.1/hansard/entries/1275858/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1275858,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1275858/?format=api",
"text_counter": 382,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kusema kweli, hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu, ina maana kwamba sarafu yetu inapungua dhamani ikilinganishwa na Dollar ya Marekani ambayo ndio sarafu inayotumika kimataifa. Baadhi ya mambo ambayo yamesababisha kupungua kwa nguvu ya sarafu yetu ni baadhi ya sera za Serikali hii ambayo tuko nayo. Serikali ilipoingia mamlakani, Dollar ilikuwa inabadilishwa kwa Kshs100; Kshs110 au Kshs120. Lakini sasa tumeona kwamba imeongezeka wa asilimia karibu thelathini katika muda mchache kabla ya mwaka mmoja kuisha. Hii inamaanisha kwamba hii Serikali lazima iketi chini iangalie ni vitu gani wanavyofanya ambavyo hawastahili kufanya."
}