GET /api/v0.1/hansard/entries/1275861/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1275861,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1275861/?format=api",
"text_counter": 385,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Tukiangalia baadhi ya marekebisho kama vile 2(b) (c) (d) na (e), zote zinasema kwamba Waziri wa Fedha atapeleka ripoti katika Bunge la Kitaifa kabla ya tarehe 30th mwezi wa nne, kila mwaka. Ina maana ile nafasi ya kuripoti itakuwa haiji tena katika Bunge la Seneti. Itakuwa inapelekwa kwa Bunge la Kitaifa pekee yake na hiyo itakuwa inakiuka Katiba katika kipengee cha 211. Kipengee cha 211(b) inasema katika muda wa siku saba baada ya kauli kutoka kwa Bunge lolote yaani Bunge la Kitaifa au la Seneti, Waziri anaweza kuitwa akaeleza ripoti ya mikopo iliyochukuliwa na vile pesa zimetumika katika mikopo hiyo. Kwa hivyo, kwa vipengee hivyo viwili, ina maana kwamba kipengee cha 211(d)(e) zote ziko kinyume na Katiba na hazifai kukubalika na Bunge hili. Jambo la tatu ni kwamba kwa sasa deni letu limewekwa takriban trillion kumi au karibu na trillion tisa nukta nane ama tisa nukta tisa. Sheria hii inajaribu kubadilisha mfumo wa deni, yaani deni iwe ni asilimia fulani ya mazao yanayotokana na nchi yetu ya Kenya. Kwa mfano, kwa sasa, mazao yako trillion kumi na tano. Tukiweka katika asilimia ya hamsini na tano, itakuja takriban trillion nane ama kiasi kama hicho."
}