GET /api/v0.1/hansard/entries/1275870/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1275870,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1275870/?format=api",
"text_counter": 394,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "ya kuongeza kiwango cha deni kulingana na jinsi wanavyotaka kisha baadaye watuambie kuwa waliongeza kwa sababu ya jua kali, uvamizi wa mashamba na nzige katika sehemu fulani au kwa sababu hakukuwa na hiki au kile nchini. Hatutaki Kipengee 2(c) kwa sababu itanyima Seneti na Bunge la Taifa nafasi ya kuhoji jinsi pesa zitakavyotumika. Ni bora Waziri aje katika Bunge na kusema anataka kuongeza deni kwa sababu fulani kisha Bunge likubali au likatae kuliko atumie pesa halafu baadaye aje aseme aliongeza deni kwa sababu, kwa mfano, alijenga makazi mapya ya Rais au Naibu wa Rais, au waliongeza Chief Administrative Secretaries (CASs) . Kwa hivyo, Kipengee 2(c) hakifai kupitishwa kwa sababu kitakiuka Katiba. Bunge lina uwezo kikatiba kuhakikisha kwamba sharia inafuata. Huu ni wakati mwafaka wa kuwa na mjadala kuhusiana na ofisi ya kudhibiti deni la umma. Kwa sasa, wadhfa huo uko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango. Madeni huathiri nchi nzima kwa sababu tukishindwa kulipa, nchi inaweza kusambaratika. Hatungependa maswala ya madeni kusimamiwa na watu ambao wameajiriwa na Serikali na kusimamiwa na Waziri wa Fedha na Mipango. Ofisi hiyo inafaa kuundwa kando ya kikatiba ili maamuzi yafanywe kulingana na sheria. Kwa mfano, the Central Bank of Kenya (CBK) ni taasisi huru ambayo hufanya maamuzi kulingana na sheria na hakuna mtu anayeweza kukataa maamuzi yao. Kwa sasa, maswala ya madeni yako chini ya Wizara ya Fedha na Mipango na maamuzi yote---"
}