GET /api/v0.1/hansard/entries/1275879/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1275879,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1275879/?format=api",
"text_counter": 403,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Hapa tunazungumzia madeni ya Serikali ya kitaifa pekee. Serikali za kaunti zikitaka kukopa, wanaambiwa kuwa hawana uwezo au wasubiri. Mara nyingi, Wizara ya Fedha na Mipango haiko tayari ku-guarantee kwamba serikali za kaunti zinaweza kukopa. Ipo haja ya kugawanywa madeni ili serikali za kaunti ziweze kukopa kiwango fulani na kiasi fulani kiwe cha Serikali ya kitaifa. Kwa mfano, Serikali kuu inaweza kukopa asilimia 70 na serikali za kaunti zikope asimilia 30 ya 55; au iwe asilimia 60 kwa 40. Hiyo itakuwa bora kwa sababu kwa sasa hatujui jinsi serikali za kaunti zinaweza kukopa kwa kuwa ni kama ni lazima wale wanaotaka kukopa wapitie kwa Serikali ya kitaifa. Kwa mfano, ikiwa mimi ndiye nafanya maamuzi kuhusu ukopaji kisha Sen. Ali Roba aniambie anataka kukopa, nitahakikisha kuwa nimeridhika kwanza kabla ya kuangalia mtu mwingine. Hivyo ndivyo Serikali ya kitaifa inavyofanya kwa sababu madeni ya serikali za kaunti yatachangia deni la kitaifa. Hiyo ina maana kwamba nafasi ya Serikali ya kitaifa kukopa itakuwa imepungua kwa sababu ya madeni yatakayokopwa na serikali za kaunti. Kuna haja ya kuwa na mazungumzo ili kujua asilimia gani ya kiwango cha deni itakuwa inakopwa na serikali za kaunti na asilimia gani itakopwa na Serikali ya kitaifa. Lazima serikali za kaunti pia zipate fursa ya kufanya maendeleo bila kushurutishwa au kuzuiliwa kwa njia moja au nyingine. Bw. Spika wa Muda, kwa kumalizia, tunaunga mkono Mswada huu lakini marekebisho lazima yafanywe. Kipengee cha kuripoti kwa Bunge la Taifa pekee kiondolewe. Jinsi tunavyojadili Mswada huu, lazima ripoti ziletwe katika Mabunge yote mawili; Bunge la Taifa na Seneti. La pili, hatukubali uwezo wa Waziri kukopa kisha baadaye aje kuuliza kibali kutoka kwa Bunge. Tutakuwa tumempa Waziri uhuru wa kupita kiasi kuweza kukopa. Hiyo itakuwa kinyume na matarajio ya nchi yetu ya Kenya. Mwisho ni kwamba lazima tuwe na mjadala kuhusiana na mambo ya ofisi huru ya kudhibiti madeni; yani independent public debt office . Tunafaa kujua asilimia ya deni ambayo serikali za kaunti na ya Serikali ya kitaifa zinaweza kukopa kwa sababu zote ni serikali ambazo zina mapato na zina haja ya kufanya maendeleo katika nyanja tofauti tofauti katika nchi yetu ya Kenya. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono lakini kwa masharti ambayo nimezungumzia."
}