GET /api/v0.1/hansard/entries/1276567/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1276567,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1276567/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Butere, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Nicholas Mwale",
"speaker": null,
"content": "Utapata kuwa mzazi anapozuiliwa, mtoto anakosa yule ambaye atashughulikia mambo ya mavazi, chakula na mahali ambapo ataishi. Ninampongeza mwenzangu ambaye ametuhimiza tuanzishe mikakati na miundo misingi ambayo itazingatia masilahi ya watoto ambao wazazi wao wamezuiliwa kizimbani kisheria. Tukitaka Kenya inawiri katika miaka ijayo, lazima tuzingatie miundo misingi mizuri itakayowasaidia watoto ambao watakuwa viongozi, wafanyikazi, walimu na madaktari wa kesho katika nchi yetu ya Kenya. Serikali inapaswa izingatie jinsi ambavyo watoto wa wazazi ambao wamezuiliwa magerezani watasaidiwa ili waende shule. Kama ni wagonjwa, lazima tujue jinsi ambavyo watapata matibabu. Pia, tujue ni vipi watapata masomo na chakula. Ninaiunga mkono Hoja hii ya mwenzangu ili watoto ambao wazazi wao wamezuiliwa wapewe kipaumbele."
}