GET /api/v0.1/hansard/entries/1276654/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1276654,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1276654/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mheshimiwa Spika wa Muda. Mimi kama mama, ninaunga Hoja hii ya leo mkono ili watoto ambao ni vipenzi na roho zetu walioko shuleni, waweze kupata dawa za minyoo. Ninakumbuka tukiwa wadogo, tulikuwa tunapewa dawa ambazo ungeketi vibaya, ungepata mnyoo ambaye ni mdudu mrefu tena wa kutisha ametoka. Tulikuwa tukilia siku hizo lakini kwa sasa, mambo yameendelea kiteknologia na madaktari wanafanya kazi yao kwa kasi. Kuna dawa nzuri ambazo watoto wakila, wale minyoo wanasagwa ndani ya tumbo ilhali mtoto anakaa vizuri. Elimu ya watoto wetu imetatizika kwa sababu watoto wengi wanatoka katika familia maskini na hawapati lishe bora. Watoto wanapoenda kucheza kwenye mchanga, wanakula matope na maisha yao ni duni... Naibu Spika wa Muda, wazazi wao wanashindwa hata na senti za kuwanunulia dawa za minyoo maanake wanaishi katika maisha ya uchochole; mama anashindwa, anunue chakula ama dawa ya minyoo?"
}