GET /api/v0.1/hansard/entries/1276659/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1276659,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1276659/?format=api",
    "text_counter": 270,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Ninaunga Hoja hii ya leo mkono kuwa shule zetu kupitia Wizara ya Afya, zinaweza kutoa hizi dawa ili watoto wapelekewe shuleni, watumie, ndio wapate afya nzuri ya kuendelea na masomo yao vizuri wakiwa na furaha, ili na sisi tutoe madaktari, marais, viongozi na watu wa tajriba kubwa kwa Taifa hili kwa sababu mtoto atakuwa amestawi katika elimu, a mefocus darasani na matokeo yatakuwa mazuri. Sehemu kubwa ya Bajeti ya Taifa hili imekuwa ikienda kwa vitu ambavyo si vya kusaidia sana. Kama mama ambaye ako na watoto sita, wakati mwingine ninapotelea Bungeni ama kazini mpaka ninasahau kuwadeworm watoto wangu kwa sababu niko mbioni nikitafuta hali ya maisha."
}