GET /api/v0.1/hansard/entries/1276660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1276660,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1276660/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Watoto wakienda shule, iwe ni shule ya kibinafsi au ya Serikali, ninaomba wachukuliwe kwa usawa. Kila mtoto shuleni apewe hii dawa ya minyoo. Tunaomba hizi dawazipelekwe kwenye shule zote maanake wanaambukizana hayo maradhi shuleni na akikuja nyumbani, anaambukiza wenzake. Kwa hivyo, inakuwa ni kitu kinachoendelea kwenye jamii. Ni furaha yangu kama mama nikiona wanangu waking’ara na kusoma kwa bidii. Watoto hawapaswi kuwa na minyoo katika shule ili Taifa hili linawiri kuanzia kwa watoto mpaka sisi wenyewe. Kama mama anayesimamia Kaunti ya Mombasa, ninapigia pondo mjadala huu wa leo. Watu kule nje wanasema mimi ninachapa Kiswahili hapa; ninawaambia kuwa watu wangu wa Mombasa wanafuraha nikizungumza nao kwa lugha ambayo wanaielewa zaidi; sio kuwa sielewi Kingereza, lakini ninazungumza lugha yenye watu wangu wanaielewa Zaidi. Kwa hivyo, wana Mombasa, huku Bungeni, tunasukuma Hoja hii ya dawa za minyoo ziletwe kwenye shule zetu ndiposa watoto wasome kwa furaha. Asante sana, Naibu Spika wa Muda."
}