GET /api/v0.1/hansard/entries/1276687/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1276687,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1276687/?format=api",
    "text_counter": 298,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": "Hili ni swala ambalo ningependa lishabikiwe na wabunge wengi, waume na wake katika Bunge hili. Tunatambua kuwa kuna shida kwa sababu ya umaskini uliokita mizizi katika jamiii zetu Kenya nzima. Ninapigia upato sehemu yangu ya Kwale nilikotoka. Eneo lile la Kwale au gatuzi la Kwale lina sehemu za uchochole na umaskini mwingi kwa jamii zilizoko pale. Nikimwangalia mtoto wa shule ambaye mzazi hawezi kununua hata kiatu, je ataweza kumuondoshea minyoo ama kumfanyia deworming yule mtoto wake? La hasha, haiwezi. Ningependa huu mpangilio ambao tunaulilia sana upatikane wa wanafunzi kufanyiwa zoezi la kuondoa minyoo au kufurushwa kwa minyoo. Ni bora jambo hili liweze kupatikana katika shule zote za Kenya. Tukiangalia shule nyingi pale Kwale ninakotoka, hata maji shule hazina. Wanafunzi wanapotoka pale tunajiuliza mikono yao hua wamejipanguza na nini au wamefanya nini. Anatoka pale mtoto anakwenda kula chakula, matunda ambapo hajasafisha wala kuosha mikono yake ipasavyo. Mhe. Spika wa Muda ninaipigia upato na ninaunga mkono Hoja hii. Taifa hili kupitia kwa Wizara ya Afya tuweze kuwafanyia watoto wetu shughuli hiyo, watoto wa miaka kumi kukuja chini, ni jambo ambalo litatuvutia sana sisi Wabunge. Litatujenga na pia tutaweza kudhibiti afya ya watoto wetu. Ukiangalia unaweza kuona mtoto amekonda kabisa, unafikiria ana maradhi gani ambayo yanamsibu lakini ni sababu ya kuwa afya yake haijaangaliwa na tunajua mtoto mdogo lazima aweze kutibiwa minyoo ndio apate afya nzuri kwa maisha mazuri. Ndio kesho na yeye aweze kusimama mbele ya Bunge hivi, aweze kuwa mtu mkubwa au Gavana lazima apate afya mzuri. Ninamuunga mkono aliyeleta Hoja hii iweze kuratibiwa na kufikiriwa na Serikali yetu ya Kenya. Asante sana. Ninaunga mkono Hoja hii."
}