GET /api/v0.1/hansard/entries/1276880/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1276880,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1276880/?format=api",
"text_counter": 186,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Zamzam Mohammed (",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hii Hoja ambayo imeletwa na mwenzetu katika Bunge hili inahusu mambo yanayoathiri mwananchi kila uchao. Katika upande wa pili, ndugu yangu alisema wanarekebisha. Hatuwezi kukaa tukisema tunarekebisha wakati mambo yanaenda kombo. Tunapoteza Ksh700 bilioni kila mwaka. Wakifanya hesabu zao, hawawezi kutupatia uhakika wamefanya kitu gani. Kama alivyosema ndugu yangu, Mhe. Waluke, ndio maana kuna miradi mingi imekwama. Ilianzishwa na iko msituni. Nyasi imemea kule wakati kuna sehemu ambapo jumba kama lile linahitajika. Wakikuja kufanya hisabati, wanapata kuwa pesa nyingi sana zimetumika pale, lakini hakuna uwajibikaji kuonyesha jinsi ilivyotumika. Hiyo ni dhahiri kuwa pesa zimeingia katika mifuko ya watu."
}