GET /api/v0.1/hansard/entries/1276883/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1276883,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1276883/?format=api",
"text_counter": 189,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Zamzam Mohammed (",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": ", zinaangaliwa vizuri na kupatiwa title deeds zao. Tukiangalia mambo ya ugavi wa kazi, kama walivyosema wenzangu nami pia natilia pondo. Kuna makabila ambayo utayaona katika kazi fulani kwa sababu, pengine mkubwa anayeongoza ni kabila lao na wengine wote wanaachwa nje. Ninazungumzia watu wangu wa Pwani. Hata kule Mombasa kuna raslimali zetu lakini wanaozimiliki na kushikilia hatamu ya uongozi ni wale walioajiriwa pale na sio sisi. Wanaotoa ajira utapata basi wanatoka sijui wapi na wanashukishwa Mombasa. Pengine ni watoto ambao wanapewa trainings badala wachukue watoto wa Mombasa; basi wanatoka sehemu nyingine na kuwamwaga kule. Hii ni kuonyesha sisi tunadharauliwa. Ningetaka kuelezea Serikali hii, vile mlivyoahidi mtatetea haki ya wanyonge, sisi twataka kuona. Kule Pwani tunamiliki asilimia 70 za raslimali zetu kama ilivyo katika Katiba. Asilimia 30 inarudi kwa wengine na hatuwezi kukataa kwa sababu ni sheria. Watoto wetu wamekosa shule za kusomea. Lakini unapata sehemu zingine hapa Kenya pengine barabara inajengwa na kipande kidogo kutoka hapa mpake pale kinachukua mamilioni ya pesa na barabara haijaisha. Mradi unaanzishwa na unapata umeduduma, pesa zimeliwa, wanabadilisha contractor na kuleta mpya. Haya ni mambo tunayopigana nayo. Tusipoangalia kwa kina, itakua Mkenya analipishwa ushuru mwingi sana lakini pesa zinaingia kwenye mifuko ya watu ambao hawana shukrani. Yule maskini atalipishwa ushuru mkubwa sana na kuna matajiri ambao wamekaa mahali na wanazidi kutajirika kila uchao na maskini anazidi kuwa maskini kila siku. Nilazima tuwe na regional balance katika mgao wowote ule. Ikiwa Mombasa ama kule Kilifi bado maendeleo hayajafika vizuri, wakiangalia ule mgao pengine watu wa Meru wameendelea vizuri. Ninasema kwa mfano ndiyo Mbunge wa Meru asinitoe jicho hapa. Ikiwa pengine maendeleo ya Nairobi yameshika kasi, basi waangalie sehemu ambazo yale maendeleo hayajafika ili waweze kuekeza huko ili Wakenya wote walipe ushuru na kila mmoja apate haki yake. Mhe. Spika wa Muda, nikimalizia, ninataka kuzungumzia mambo ya elimu, docket ya"
}